NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imetangaza kutoa huduma ya tiba ya mifupa na viungo kwa watoto bure siku ya Jumatano Mei Mosi,2024
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Aprili 29,2024 na Meneja Uhusiano wa Moi,Patrick Mvungi,Wazazi na walezi wenye watoto wenye matatizo ya mifupa na viungo wanaarifiwa kuwaleta katika taasisi ya MOI.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa muda ni kuanzia saa 2:00 asubuhi ili kupata huduma za Madaktari Bingwa wa Mifupa.