NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani hapa leo Aprili 29, 2024.
Katika Ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua miundombinu ya barabara, madaraja na maeneo mengine yaliyoathiriwa na mvua pamoja na kukagua hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Mamlaka huska katika Sekta ya Ujenzi.
Waziri Bashungwa atatembelea barabara ya Kibada – Mwasonga, barabara ya Mji Mwema – Pembamnazi, barabara ya Kigamboni – Kibada, barabara ya Mwaikibaki, barabara ya Mbezi Victoria – Mpiji Magoe pamoja na utoaji huduma wa Vivuko vya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).