NA MWANDISHI WETU, RUFIJI
MKUU wa wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele,amevitaka vyama vya siasa nchini kuiga matendo yanayofanywa na Chama cha ACT Wazalendo cha kuwakimbilia na kuwasaidia waathirika wa mafuriko katika wilaya hiyo badala ya jukumu hilo kuachwa kwenye mikono ya serikali peke yake
Meja Gowele alitoa kauli hiyo jana wakati akipokea misaada ya vyakula nguo, mataulo ya kike beseni na mafuta kutoka kwa kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo,Doroth Semu,aliyefika wilayani humo kwa ajili ya kujionea athari za mafuriko
“Mwanzo alipita hapa Waziri Mkuu Kivuli wa Chama chenu,alitukosoa na kutoa ushauri wan jia sahihi ya kutatua hizi changamoto kwa dharura,matokeo ya ziara ile walifika viongozi mbali mbali wa serikali hapa na ninyi leo mmekuja kwa mara ya pili sit u kutukosoa lakini mmeleta misaada kwa waathirika naomba na vyama vingine vya siasa viige mfano huu”alisema Meja Gowele.
Awali kabla ya kukabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya Semu aliyeambaatana na ujumbe wake alikutana na mkuu wa mkoa wa Pwani,Abubakar Kunenge na kumueleza kuwa ni muhimu ifanyike tathmni ya kina kwa waathirika na kisha wafidiwe
Alisema Mafuriko ya Rufiji na Kibiti yanapaaswa kutazamwa kwa jicho la ziada kutokana na kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na matokeo ya kufunguliwa kwa maji katika mradi wa kufua Umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere.
Rufiji na Kibiti wamekuwa waathirika wakubwa wa mafuriko hayo kutokana na kutokuwepo kwa mipango sahihi ya matumizi ya maji yaliyotoka katika Mabwawa ya Mradi wa kufua Umeme wa Mwalimu Nyerere,lengo la Pili la Mradi ilikuwa ni kuwawezesha wananchi kufanya kilimo cha Umwagiliaji kwa kujenga mabwawa ya ziadaa ambayo mpaka sasa hayajajengwa”alisema Semu
Aliongeza kuwa ni wakati sahihi kwa Serikali kufanya tathmini ya Kina na kuhakikisha kila Mwananchi aliyeathiriwa na mafuriko hayo anapatiwa fidia kutoka na ukubwa wa madhara aliyopata
Alisema ACT Wazalendo kwa nafasi yake ya Chama cha siasa wamefika Rufiji kwa ajili ya kuwafariji waathirika na watafurahi kuona wananchi wanaanlipwa kutokana na athari walizopata
Miongoni mwa misaada waliyoitoa ni vyakula, nguo, sabuni, mafuta ya kula, vyombo na kwamba kwa ujumla wake ni vya tani tatu vyenye Sh.milioni 6.5.
Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa,Isihaka Mchinjita kwa upande wake,alisema nchi inapaswa kujifunza katika mafuriko ya Rufiji kabla ya madhara makubwa hayajatokea n ani vema wakafanya kazi kutokana na ushauri wa wataalamu waelekezi
Alisema mwaka 2020 kingo za bwawa la Nyerere lilibomoka na ilipsawa wakat huo kuwa darasa tosha kabla ya madhara makubwa zaidi hayajaajitokeza ikiwa bwawa litapasuka kama ilivyotokea Libya