NA MWANDISHI WETU, KATAVI
MAHAKAMA ya Wilaya ya Tanganyika imemuhukumu Ntunga Sahani, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kagunga Kata ya Kasekese, Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh.500,000 kwa kosa la kupokea hongo ya Sh.320,000.
Kosa la Mwenyekiti huyo wa Kijiji ni kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya mwaka 2022.
Kesi hiyo ya jinai namba CC. 9586/2024 kwa upande wa Jamhuri iliongozwa na Hakimu Mfawidhi Sydney Nindi
Akisoma hati ya Mashtaka, Mwendeaha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Vailet Achimpota alisema, Mshtakiwa huyo kwa tarehe tofauti kati ya Juni 1, 2023 hadi Julai 30, 2023 alipokea hongo hiyo kutoka kwa Wanakijiji 16 wa Kijiji cha Kagunga, Kata ya Kasekese, ili awagawie mashamba katika maeneo ya hifadhi ya Msitu wa Kalaba uliopo Wilaya ya Tanganyika.
Mshtakiwa alikiri kosa lakini alishindwa kulipa faini iliyoamriwa na Mahakama hivyo yupo gerezani.