Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, pamoja na baadhi ya Mabalozi wa Nchi Sita Marafiki za Kusini mwa Afrika, wakiwa wamesimama kimya kwa dakika moja, kuomboleza na kumkumbuka aliyekuwa Rais wa Namibia, Hayati Komredi Hage Gottfried Geingob, kabla ya kuanza mazungumzo yao kuhusu masuala mbalimbali, yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar Es Salaam. Kulia kwa Dk. Nchimbi ni Balozi wa Angola, Sandro de Oliveira, akifuatiwa na Balozi wa Msumbiji. Ricardo Mtumbuida na anayefuata ni Balozi wa Afrika ya Kusini, Noluthando Mayende-Malepe. Nchi zinazounda urafiki huo wa kihistoria na Vyama Sita Rafiki vya Ukombozi wa Kusini mwa Afrika, vinavyoongoza nchi hizo ni Tanzania (CCM), Angola (MPLA), Msumbiji (FRELIMO), Zimbabwe (ZANU – PF), Namibia (SWAPO) na Afrika Kusini (ANC).