NA MWANDISHI WETU, KIBAKWE
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene amesema kukatika kwa Daraja la Kidunda kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mengi hapa nchini kumeleta adha kubwa kwa jumla ya Kata 13 za za Jimbo hilo huku huku akiwashukia wananchi wanaoharibu mazingira kwa kulima na kukata miti maeneo ya milimani kuwa ndo chanzo cha tatizo hilo.
Amesema Daraja hilo linalounganisha upande wa Kusini mwa Jimbo la Kibakwe ni muhimu kwa wakazi wa meneo hayo kwani hutumiwa kwa ajili ya shughuli za usafiri kwa wananchi wote wanaokwenda katika wilaya ya Mpwapwa.
Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Februari 4, 2023 wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Kibakwe, wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma mara baada ya kutemmbelea daraja hilo lililokatika hivi karibuni ambapo tayari TARURA wilaya ya Mpwapwa na TANROADS mkoa wa Dodoma wapo eneo la tukio kwa ajili ya matengenezo
Akizungumza na wananchi hao, Simbachawene ametoa pole kwa wakazi wa Kibakwe kwa adha wanazopata kutokana na kukatika kwa mawasiliano kulikosababishwa na kukatika kwa Daraja hilo
Ametumia fursa hiyo kuwatoa wasiwasi wakazi hao wa Kibakwe kuwa Mkandarasi anayeendelea na utengenezaji wa Daraja hilo atafanya kazi ya kuhakikisha daraja hilo linakamilika kwa wakati
” Nawashuukuru sana TARURA Mpwapwa na Tanroads mkoa wa Dodoma kwa utayari wao toka Januari 31, 2024 Daraja hili lilipokatika walifika kuhakikisha utengenezaji wa daraja mpya linaanza mara moja.
Vile vile, Simbachawene ameagiza viongozi kuanzia ngazi ya Mtaa hadi wilaya pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuhahakisha hakuna wananchi wanakata miti na wala kulima juu ya milima na hivyo kusabisha mvua inaponyesha hupelekea maji kushuka kwa kazi sana katika maeneo ya tambarare
Amesema katika Jimbo la Kibakwe madaraja yaliyo mengi yameharibiwa kutokana na jimbo hilo kuzungukwa na milima pande zote hivyonkitendo cha wananchi kulima juu ya milima hiyo kunachochea tatizo kuwa kubwa zaidi pindi mvua nyingi zinaponyesha
Amewataka wananchi waache kulindana kwa uharibifu huo wa mazingira una athari kwa watu wote wanaoharibu mazingira na wale wasio haribu huku akisisitiza kuwa mvua zinazoondelea kunyesha zinatoa fundisho juu ya umuhimu wa kutunza mazingira
Diwani wa Kibakwe David Chisanza amesema changamoto hii ya uharibifu wa mazingira ndio sababu iliyopelekea daraja kukatika, kuna watu wamekamatwa na wamepelekwa Mpwapwa lakini kesi zao zimekuwa zikiishia juu kwa juu nakuomba utusaidia kwani tusipochukua hatua hii Kibakwe itaisha