NA MWANDISHI WETU, BUTIAMA
WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ametembelea Butiama kwa ajili ya kuzuru Kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kutembelea Makumbusho yake katika kijiji cha Mwitongo, Wilayani Butiama Mkoani Mara.
Bashungwa amepata nafasi ya kuongoza dua ya kumuombea Baba wa Taifa, Kuwasha mshumaa pamoja na kuweka mashada ya Maua katika kaburi la Baba wa Taifa.
Pamoja na mambo mengine amepata nafasi ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kumbukumbu katika Makazi ya Baba wa Taifa katika kijiji cha Mwitongo.
Waziri Bashungwa anaendelea na ziara ya kikazi katika Mikoa ya Mbeya, Iringa, Singida, Simiyu na sasa yupo Mkoa Mara ambapo atatembelea na kukagua miradi na shughuli mbalimbali zianzoendelea katika Sekta ya Ujenzi.
Sambamba na hilo Bashungwa amesema kazi kubwa aliyoifanya Baba wa taifa ni ya kukumbukwa huku akiwahamasisha watanzania kujenga tabia ya kujifunza mambo mema kwa waliotangulia.









Waziri huyo amesema kazi kubwa aliyoifanya baba wa taifa ni kujenga misingi ya kupendana na kuheshimiana huku akiwa mstari wa mbele kuhimiza watu kufanya kazi kwa bidii.
Aidha amesema licha ya Baba wa taifa kupambana ili kutafuta uhuru wa wa Tanganyika pia alipenda amani ya nchi sambamba na kila mmoja kumuheshimu mwingine na kuondokana na vitendo vya ukabila,dini au rangi ya mtu.