NA MWANDISHI WETU, MWANZA
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (Tasac) limetangaza kuanza operesheni maalumu kudhibiti tabia ya baadhi ya vyombo vya usafirishaji majini kuzidisha idadi ya abiria.
Operesheni hiyo itakayfanyika katika mialo na bandari za Ziwa Victoria inathusisha hatua za kisheria dhidi ya manahodha na wamiliki wa vyombo vitakavyokutwa vimezidisha abiria kinyume cha sheria, lengo likiwa ni kulinda usalama wa vyombo na maisha ya abiria wakati wa safari.
Ofisa Mwandamizi Ukaguzi wa Meli kutoka Tasac, Ghadaf Chambo amesema uamuzi huo unatokana na baadhi ya vyombo vya usafirishaji kuzidisha abiria, hali inayohatarisha usalama vyombo,mali na maisha ya abiria.