DAR ES SALAAM, TANZANIA
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imelaza timu ya taifa ya Niger kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa kutafuta kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika (Afcon)
Bai pekee la Stars liliwekwa kambani na Simon Msuva dakika ya 69 ya mcheza baada ya kuitumia vizuri krosi iliyomkuta akiwa katikati ya walinzi.
Kwa ushindi huo, Stars imechupa mpaka nafasi ya pili iliwa na alama 7 nyuma ya vinara Algeria wenye alama 12.
Sala za Watanzania zinaelekea kwenye mcezo kati ya Algeria na Uganda ambao ndio utaamua kama Stars iende Afcon au la.
Kama Uganda yenye alama nne ikifanikiwa kuifunga Algeria basi Uganda itafuzu na Stars itabidi isubiri mpaka mwaka 2025