NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MMILIKI wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW)Michael Shirima amefariki dunia katika hospitali ya Aga Khan alipokuwa akipatiwa matibabu tangu alipolazwa Juni 8 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Tangazo lililotolewa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Shirika hilo Hillary Mremi , mapema asubuhi ya leo Juni 10, 2023 kupitia mitandao ya kijamii limethibitisha kifo cha Mmiliki huyo kilichotokea Juni 9, 2023 katika hospitali hiyo.
Taarifa zaidi zitawajia kadri tutakavyozipokea.