NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAKALA wa Usajili wa Biashara (BRELA) leo Juni 8,2023 imefanya Kikaokazi na Wahariri wa Vyombo Mbalimbali vya Habari na Jukwaa la wahariri Tanzania(TEF) jijini Dar es salaam kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu Mmiliki Manufaa .
Akizungumza katika kikao kazi hicho Kaimu Mkurugenzi wa Makampuni na Majina ya Biashara wa BRELA , Meinrad Rweyemamu amesema dhana ya Mmiliki Manufaa inakuja kufuatia marekebisho ya sheria ya Makampuni sura ya 212 kupitia sheria ya fedha ya mwaka 2020.
Aidha Rweyemamu amesema kwamba marekebisho hayo yamekwenda sambamba nautungwaji kanuni za Wamiliki Manufaa mwaka 2021 kusimamia ukusanyaji na utoaji taarifa manufaa wa Kampuni.