NYOTA wa zamani wa klabu ya Barcelona na Manchester City, Yaya Toure ametoa neno hujuma walizofanyiwa Yanga kwenye mchezo wa finali dhidi ya USM Alger na kulitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchukua hatua.
Wakati umefika kwa mashabiki wa soka wa nchi zetu barani Afrika kuitaka CAF kuwa na mechi moja pekee ya fainali kwenye uwanja usiofungamana na upande wowote (neutral).
Ni aibu kwa bara letu kuona udhalilishaji wa timu ya ugenini (Yanga) kukumbana na mashambulizi ya kuvizia kwa fataki nyakati za usiku wakiwa wanashambulia lango la wenyeji.” alisema Yaya
Nguli huyo wa soka Afrika kutoka Ivory Coast alisema ni fedheha kuona wakati wa mchezo vijana waokota mipira (ball boys) wakirusha mipira mingi kwa wakati mmoja ili kupoteza muda kwa ajili ya timu za nyumbani, zaidi ya fataki mbili nzito zilipigwa kiasi cha kupelekea mechi kusimamishwa (mara tatu) ili kuruhusu moshi huo kutoweka, yote haya yalifanywa mbele ya rais wa CAF na ulimwengu mzima wa mashabiki wa soka wakitazama.
Yaya alilalamika na kusema sio mara ya kwanza barani Afrika kushuhudia mambo ya hovyo yanatatokea na bila hatua yoyote kuchukuliwa