NA MWANDISHI WETU, KOROGWE
SERIKALI wilayani Korogwe mkoani Tanga imeonya kuwa hatosita kuwachukulia hatua kali za kisheria dhidi ya wale wote ambao watahujumu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo wa BOOST.
“Hatuta vumilia mtu yoyote ambaye atapuuzia utekelezaji wa nia njema ya Rais wa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Korogwe kwa kutotekeleza miradi kwa wakati husika na kwa viwango vinavyotakiwa na Serikali”
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo ameyasema hayo akizindua rasmi Kampeni Maalumu ya Oparesheni Samia (OP SAMIA KOROGWE)
mara baada ya kuungana na wananchi kuchimba msingi katika Shule ya Msingi Magila Gereza, Kata ya Magila mjini Korogwe Mei 31, 2023.
“Madhumuni ya Kampeni hii ni kuwa na utekelezaji kusimamia miradi kwa uwazi na bidii kwa mujibu sheria kanuni na utaratibu husika wilayani hapa” alisisitiza zaidi
Amewataka watumishi kukataa na kutokuwa sehemu ya ubadhirifu wa fedha za umma katika utekelezaji wa miradi ya serikali.
Aidha amewataka waratibu na watendaji wa miradi kushirikiana na wananchi hasa katika maeneo yao ya miradi.
Kauli Mbinu ya kampeni hiyo ni ‘Maliza Miradi, Kazi Iendelee’.