NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa ,Isaack Mnyangi (45) aliyemjeruhi kwa kumng’oa meno na jicho kwa plaizi na bisibisi Mkewe Jackline Mnkonyi.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Justine Masejo, mtuhumiwa huyo alitiwa mbaroni jana eneo la Himo mkoani Kilimanjaro alipokuwa amejificha kukwepa mkono wa sheria.