NA VICTOR MASANGU, MAFIA
WANANCHI wa Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani wamemshukuru Rais wa awamu ya sita Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya ,elimu na maji.
Haya yameeekezwa kwa nyakati tofauti wakati wa ujio wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipowasili wilayani Mafia kwa ajili ya kutembelea ikiwa sambamba na kukagua,kuzindua,na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo.
Mmoja wa wananchi hao Amina Tuki amesema kwamba ujio wa Mwenge wa Uhuru ni mkombozi mkubwa katika kuchochea kasi ya maendeleo na wananchi kuweza kupata fursa ya kupata huduma za kijamii kwa urahisi.
Aidha amepongeza juhudi zilizofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Mafia kwa kufanikisha mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa mahututi (ICU) pamoja na jengo la dharura.
“Kwa kweli tunashukuru sana ujio wa Mwenge wa Uhuru umeweza kuja na kutembelea miradi yetu ya maendeleo sisi kwetu imeweza kutusaidia wananchi kutokana na kuwepo kwa huduma ambazo tunazipata kama vile,maji,afya,elimu na mambo mengine muhimu,”amesema
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Abdallah Kaim amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Mafia kwa kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.
Kadhalika kiongozi huyo amewahimiza watendaji na viongozi kuitunza na kuilinda miradi ambayo wameianzisha ikiwa sambamba na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dk.Samia.
Pia amebainisha kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuendekea kuwafikishia huduma za Afya Kwa ukaribu wananchi wake Ili kuondokana na gharama kubwa kwa ajili ya kupata matibabu.
Akipokea Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mafia Zephania Sumaye amesema mwenge huo utakimbizwa kilomita 99.8 na utatembelea, kuzindua, Kufungua,na kukagua miradi mbali mbali.
Awali akisoma taarifa ya mradi wa jengo la wagonjwa mahututi Mganga Mkuu wilaya amesema Mradi huo umegharimu Kiasi cha Milioni 564 lengo ikiwa kuboresha huduma za Afya pia majengo haya yatapunguzo vifo visivyo vya lazima kupunguza gharama za rufaa kwa Wananchi
Naye Mbunge wa Jimbo la Mafia Omary Kipanga amempongeza Rais wa awamu ya sita Dk Samia kwa kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali ya maendeleo na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na wananchi wake katika kuwaletea mabadiliko chanya.