NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WANANCHI wa baadhi ya maeneo katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani watakosa huduma ya umeme kwa siku mbili kuanzia leo Mei 20, 2023.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetaja sababu kuwa njia kuu ya kusafirishia umeme namba moja ya msongo wa kilovati 220 kutoka Kidatu hadi Morogoro itazimwa ili kumruhusu mkandarasi anayejenga mradi wa njia ya kusafirishia umeme ya treni ya mwendo kasi (SGR) kati ya Morogoro na Dodoma kufanya kazi ya maboresho ya miundombinu.
Aidha TANESCO imefafanua kuwa zoezi la kukata umeme litaanza saa 11 alfajiri hadi jioni muda huo na kuathiriwa baadhi ya maeneo ya mikoa hiyo kuanzia leo hadi kesho