NA DENIS SINKONDE, SONGWE
JESHI la polisi mkoani Songwe linamshikilia Bahati Erasto , mkazi wa eneo la Ichenjezya ,wilayani Mbozi kwa tuhuma za kumbaka mtoto wake wa kumzaa.
Kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa Theopista Mallya , amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni mlinzi wa shule ambayo haikutajwa jina amekuwa akifanya vitendo hivyo katika eneo lake la lindo pindi binti huyo anapompelekea chakula.
Kamanda huyo amesema mtuhumiwa alimbaka mtoto huyo mwenye umri wa miaka 15 majira ya sita usiku, baada ya kuingia chumbani kwa binti huyo licha kukataa akidai anaumwa.
“Katika kufuatilia siku hiyo haikuwa mara ya kwanza kwani kila mda motto huyo akitumwa na mama ake mzazi kumpelekea chakula kwenye lindo na kufanya naye mapenzi” amesema Kamanda Mallya.
Kamanda Mallya amesema mama mzazi wa mtoto huyo alibaini kitendo hicho baada ya mtoto huyo kupiga kelele akilazimishwa kufanya mapenzi na baba yake ndipo mama yake akamkuta mume wake anataka kumbaka huyo mtoto.
Kamanda Mallya amesema mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamni pindi upelelezi utakapokamilika.