NA MWANDISHI MAALUM, DAR ES SALAAM
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kukutana na kamati ya wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, Mawaziri wa sekta husika na Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA).
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Saa 8 Mchana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu MAGOGONI- ikulu
Jumatano Mei 17 , 2023 kwa uratibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla.
Kwa sasa Serikali inaendelea kuwasihi wafanyabiashara wa soko hilo kuendelea na shughuli zao za biashara wakati Serikali inajiandaa kukutana nao kwa lengo la kuwasikiliza na kushughulikia kero zinazowakabili.