NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KIASI cha Shilingi Bilioni 19.2 za Ubalozi wa Uswisi kupitia Mfuko wa kuwezesha wajasiriamali nchini, kinatarajia kutolewa ili kukuza biashara ndogo na za kati na zenye kwa lengo la kuleta matokeo chanyana kuboresha maisha ya Watanzania hususani vijana na wanawake.
Kiasi hicho kitachazosaidia wafanyabiashara ndogondogo na za kati zitasimamiwa na utatekelezwa na taasisi ya Usaidizi wa Biashara Ndogo (SEAF) kwa kushirikiana na Taasisi ya AlphaMundi (AMF).
Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Didier Chassot akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mei 10, 2023 wakati wa uzinduzi wa mfuko wa DARAJA IMPACT FUND amesema kuwa Serikali ya Uswisi inalenga kukuza biashara mbalimbali zilizopo kwenye mnyororo wa thamani na itatoa mchango wake katika maendeleo endelevu ya Tanzania.
Amesema kuwa Sekta ya binafsi inachukua jukumu muhimu wakati wa kukuza uboreshaji wa biashara zenye matokeo chanya kwenye jamii pia Mfuko huo utakuwa ni kichocheo cha ukuaji wa kiuchumi nchini.
Pia ubalozi utahakikisha kuwa kunakuwa na mfumo thabiti wa Kukuza biashara zinazogusa maisha ya jamii na mfuko huu utahakikisha unatumika kusaidia kukuza biashara pamoja na ufadhili unaohitajika ili kuongeza thamani ya biashara kuwa zenye sifa na kutimiza mahitaji ya jamii inayowazunguka.
Amesema kuwa Mfuko huo wa Daraja Impact Fund utasaidia wajasiriamali hapa nchini kuwajengea uwezo na kupata ujuzi wa kuendesha biashara zao, kuimarisha utendaji wao katika maeneo yao ya biashara na kuleta matokeo chanya ndani na nje ya biashara wanazozimiliki.Mfuko huo utatoa vipaumbele katika biashara zinazoongozwa na wajasiriamali wanawake na vijana, pamoja na biashara zenye wafanyakazi wengi wanawake au wateja na vilevile wasambazaji.
“Uswisi inajulikana kama ubozi katika eneo la ‘impact-linked financing’. Hivyo, Serikali ya Uswisi itatumia utaalamu ulionao na usaidizi wake katika kuimarisha uwekezaji wa Sekta binafsi unaokuja Tanzania, unaolenga makampuni na biashara mbalimbali zilizopo Tanzania na itatumia mbinu mbalimbali ili kukuza biashara.” Ameeleza
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mipango wa Kimataifa wa SEAF, Peter Righi amesema kuwa mfuko huo utatoa fursa kwa wafanyabiashara wa Tanzania kupata mafanikio ya kibiashara huku wakiwa na matokeo chanya katika jamii zao.
Amesema mfuko huo utajikita katika usaidizi wa kiutendaji kabla na baada ya uwekezaji na kuilimarisha utendaji wa kifedha na kukuza ukuaji wa biashara.
Wakati huohuo, Mkurugenzi Mtendaji wa AMF Ladé Araba amesema”Tunafuraha kusimamia uwekezaji wa Mfuko huu wa kusaidia wafanyabishara ili kukuza na kuimarisha zile biashara ambazo zinaonyesha uwezo wa juu wa kuleta matokeo chanya zinazomilikiwa na wanawake na vijana, huku zikitoa utendaji mzuri wa biashara.”amesema
Amesema kuwa wanasubiri kwa hamu matokeo chanya yatakayokuja baada ya ufadhili huo, uwekezaji unachagiza na kutoa ufadhili kwenye maeneo mbalimbali hususani sehemu ya mitaji kwa wafanyabiashara katika utekelezaji wa mradi huo unaofadhiliwa na Ubalozi wa Uswizi hapa nchini.
Akizungumzia kuhusiana na Ubalozi wa Uswisi, amesema kuwa imesaidia miradi mingi ya kimkakati katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania tangu mwanzoni mwa miaka ya 1960.
Mwaka 1981, Tanzania ikawa nchi ya kipaumbele yenye kupokea usaidizi rasmi wa maendeleo wa Uswisi.
Amesema mpango wa ushirikiano wa Uswisi Tanzania 2021 – 2025 unalenga kuwawezesha vijana, hasa wanawake ili kujiendeleza kijamii na kiuchumi kupitia matokeo matatu ya kisekta ambayo ni kuimarisha taasisi za serikali, kukuza nafasi zao kiraia na kuboresha maisha ya vijana