NA MWANDISHI WETU, TANGA
MKUU wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba leo Mei 11, 2023 amefanya ziara katika wilaya ya Mkinga ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea katika wilaya za mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na watumishi pamoja na kamati ya fedha na uongozi
Akizungumza wilayani humo RC Kindamba amewataka watumishi kujituma na kufanya kazi kwa juhudi huku wakisimamia ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa miradi ya maendeleo huku wakizitatua kero za wananchi kwa wakati katika maeneo yao