NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
TIMU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Tanzania imeiadhibu Marumo ya Afrika Kusini kwa magoli 2-1 kwenye nusu fainali ya kwanza ya michuano ya Shirikisho la CAF iliyochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar leo Mei 10, 2023
Ikiwa imeanza kwa kujihami kwa kuweka viungo wakabaji wengi, Yanga ilianza taratibu mchezo huo huku muda mwingi ikiwa inawasoma wapinzani wake.
Hadi Mwamuzi wa Mchezo anapuliza kipenga kuashiria kumalizika kwa dakika 45 za mwazo, si Yanga wala Marumo waliofanikiwa kuzifumania nyavu za mwenzake.
Dakika ya 64 ya mchezo, Ki Aziz alikwamisha mpira wavuni kwa shuti kali baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Tuisila Kisinda TK Master.
Dakika chache baadae, mwalimu wa Yanga, Nabi alifanaya mabadiliko na kuwatoa viungo wakabaji na kuwaingiza viungo washambuliaji ambao waliuchangamsha mchezo na kufanya wapinzani wao wawe kwenye nyakati ngumu.
Bernard Morrison aliifungia Yanga bao la pili kwenye dakika ya 92 baada ya kufanya kazi kubwa ya kupambana na walinzi na goli kipa wa Marumo.
Kwa matokeo hayo, Yanga imeingiza mguu mmoja ndani kuelekea fainali za mashindano hayo.
Hii ni mara ya kwanza kwa Yanga kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano ya klabu Afrika.