NA MWANDISHI WETU, MBEYA
WAKAZI wa mkoa wa Mbeya wameiomba Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kusambaza zaidi elimu juu ya utumaji rasmi wa mizigo na vifurushi ili kuwanusuru wananchi wengi zaidi na upotevu wa mizigo.
Wakizungumza katika kampeni ya wazi ya uhamasishaji wa matumizi ya watoa huduma rasmi wakati wa kutuma mizigo wananchi hao wamesema mizigo migo inapotea kutokana na kutojua taratibu rasmi za kuwatambua watoa huduma wenye leseni.
Akizungumzia elimu hiyo mfanyabiashara Anangisye Mwakyoma amesema mara nyingi anapotaka kutuma mizigo huangalia basi ambalo analijua lakini baada ya kupata elimu hii atazingatia maelekezo ambayo yametolewa.
Akizungumzia faida ya elimu Kissa Mwaipyana amesema iwapo angepata elimu hii tokea awali asingepoteza mzigo ambao alituma kwenye basi kupitia wakala ambaye hakuwa na ofisi.
Mchungaji Elibariki Mmari ameishauri TCRA kuweka wazi sifa na vigezo vya wasafirishaji rasmi ili wananchi wawe wanaangali hivyo kabla ya kutuma mizigo yao.
Awali akitoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutumia watoa huduma wenye leseni wakati wa kusafirisha mizigo Meneja wa TCRA wa kanda ya nyanda za juu kusini Mhandisi Asajile John amesema TCRA inapotoa leseni hutoa pia masharti na vigezo ambavyo watoa huduma hao hutakiwa kuvizingatia.
Amevitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na kampuni kiwa ofisi rasmi na kutoa risiti wanapoagiza ya mizigo wanauosafirisha.
Elimu hii ni sehemu ya kampeni ya tuma chap kwa usalama inayoendeshwa na TCRA nchi nzima kuelimisha wananchi umuhimu wa kutumia wasafirishaji wa mizigo waliosajiliwa