NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MAKAMU wa Rais wa Chama cha Wakunga nchini, Loveluck Mwasha amesema kwa siku wanawake 30 wanapoteza maisha kutokana na changamoto za uzazi.
Akizungumza leo Mei 6, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo hufanyika Mei 5 kila mwaka imewakutanisha wakunga na ya wadau mbalimbali kujadili changamoto na jinsi ya kuzitatua.
“Takwimu za vifo vya mama na mtoto bado vipo juu tunaongelea vifo 350 katika vifo 100, 000 ipo juu ama vifo vya wachanga kwenye 23 hadi 24 katika kila vizazi 1000 hivyo bado ni vifo vyingi,” amesema Mwasha.
Amefafanua kuna vifo 2030 ambavyo si vya lazima vinatokana na kumwagika damu nyingi wakati wa kujifungua au baada ya muda mfupi kujifungua na matatizo ya presha kuwa juu.
Mwasha amesema suala la mama na mtoto bado ni changamoto kubwa nchini na bado hawajafika kiwango kinacho kubalika.
“Ni zipi changamoto na nini kifanyike kama wadau kuondoa changamoto na kupunguza vifo vya mama na mtoto Moja wapo kuwapatia elimu bora wakunga,”amesema.