KAMPALA, UGANDA
POLISI jijini Kampala nchini Uganda wamewakamata maofisa 10 wa polisi kwa tuhuma za kuiba shilingi milioni 5.4 fedha za Kenya kutoka kwa wezi walioiba shilingi milioni 15.
Wanaume watatu waliokuwa kwa pikipiki walimpora raia mmoja wa Burundi begi lililokuwa na pesa hizo eneo la Makindye, jijini Kampala.
Raia huyo wa Burundi ambaye alikuwa na pesa hizo kwa sarafu za dola za Marekani na Euro alizimia baada ya kuporwa begi lake akitoka ofisi ya kubadili sarafu.
Wasamaria wema walimsaidia kurejea kwa miguu yake kabla ya wahisani wao hao kupigia simu maafisa wa polisi kuhusu tukio hilo na maafisa wa kituo cha Polisi cha Katwe kuanza oparesheni.
Inaarifiwa kuwa bila kuwajulisha wakubwa wao wala kuandikisha operesheni hiyo kwa mujibu wa kanuni, maofisa hao waliwakamata washukiwa eneo la Masajja taarafa ya Makindye.
Maofisa hao walipata pesa hizo na kuwatia mashukiwa katika seli kisha sasa wakaamua kuelekeza kesi kwa wenzao wa Idara ya Upelelezi wa Jinai.
Mambo yalikuwa sawa hadi pale ambapo washukiwa waliwaambia wapelelezi kuwa maofisa waliowakamata walisema kiwango kidogo kuliko walichowakuta nacho.
Maofisa hao walishikwa mara moja na kufungiwa katika kituo cha polisi cha Katwe ambako walikuwa wamewafungia washukiwa wa wizi waliokamatwa Makindye