NA MWANDISHI WETU, MARA
MKUU wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali, Suleiman Mzee amesusa kuweka jiwe la msingi katika ofisi za Machinga Mkoa wa Mara ofisi zilizogharimu kiasi cha Shilingi millioni 45, na kutoa siku tatu 3 kwa manispaa ya Musoma kuhakikisha inachora upya ramani ya jengo hilo na kuanza ujenzi mara Moja.
Ametoa kauli hiyo alipotakiwa kuweka jiwe la msingi katika jengo hilo na kubaini kuwa jengo hilo halikidhi mahitaji ya wafanyabiashara wadogo kutokana na ufinyu wa vyumba.
Mzee amewataka kubadili ramani na kusanifu jengo hilo kwa weledi, ikiwemo kuweka vitega uchumi, ambavyo vitaweza kuongeza kipato katika jengo hilo sasa na badae.
“Hamuwezi kujenga ofisi ya mita mbili kisha ikapewa hadhi ya mkoa hivyo mnatakiwa kubadili ramani kutokana na ukubwa wa kiwanja zingatieni muda niliowapa,”amesema Mzee.