Mshambuliaji wa PSG na time ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi (35), anaweza kwenda kucheza soka Uarabuni ambako anakipiga hasimu wake, Mreno, Cristiano Ronaldo (38) kwa uhamisho wa Pauni Milioni 320. Klabu ya Al-Hilal imeonesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo amable pia anawindwa na klabu ya Inter Miami inayoshiriki Ligi Kuu Marekani, inayomilikiwa na nyota wa zamani wa Manchester United na Uingereza, David Beckham.
Real Madrid wako kwenye mazungumzo kuhusu kumnunua kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham (19), lakini klabu hiyo ya Ujerumani inasema bado haijapokea ofa kutoka kwa wababe hao wa Uhispania. (Sky Germany)
Sheikh Jassim amesema kama ataanikiwa kuinunua klabu ya Manchester United atawasajili nyota watatu wa Ufaransa; Kylian Mbappe (24) wa Paris St-German, Kingsley Coman (26) wa Bayern Munich na Eduardo Camavinga (20) wa Real Madrid.