NA MWANDISHI MAALUM, ZANZIBAR
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi amemteua Dk Said Khamis Juma kuwa Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Taarifa iliyotolewa leo Mei, 2023 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Ikulu ya Zanzibar, Zena Ahmed Said imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza rasmi leo.
Kabla ya uteuzi huo, Dk Said Khamis Juma alikuwa Ofisa Mdhamini Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu za Serikali Pemba.