NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WADAU wanaohusika na utalii nchini wametakiwa kutoa huduma za viwango ili kuwafanya watalii kuwa mabalozi baada ya kuja Tanzania na kurudi kwenye nchi zao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damas Mfugale amesema hayo leo Mei 2, 2023 jijini Dar es salaam.
Mfugale amesema ” unaweza ukatangaza vivutio vya utalii wakaja nchini, lakini baada ya kuja uzoefu unaweza ukawa sio mzuri, ikawa hawawezi kurudi tena,”.
Amesisitiza kuwa wanaotoa huduma waongeze viwango ili watalii waweze kurudi wawe mabalozi wazuri.