NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
MAWAZIRI wa michezo kutoka nchi 14 za Kanda ya IV ya Afrika wanatarajia kukutana Jijini Arusha kuanzia Mei mosi mwaka huu kujadili namna ya kuboresha michezo katika ukanda huo. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Pindi Chana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Yakubu alisema kuwa Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano huo baada ya kutuma maombi ya kuwa mwenyeji na kukubaliwa.
Yakubu alisema kuwa Mkutano wa Baraza la Michezo la Afrika Kanda ya IV ngazi ya mawaziri mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2018 nchini Uganda, kabla ya kuzuka kwa ugonjwa wa COVID 19 na kuharibu mambo mengi mkutano huo utakutanisha wageni zaidi ya 100 kutpka ukanda huo.
Alisema baraza hilo ni chombo cha Umoja wa Afrika{AU} kinachoshughulikia michezo na kuna kanda nyingine mbalimbali ndani ya baraza hilo zinazojumuisha nchi nyingine ambazo ni wanachama wa AU.
Katibu mkuu amesema washiriki wa mkutano huo ni mawaziri wa michezo kutoka katika nchi hizo 14 ambao ni wanachama wa baraza hilo Kanda ya IV na mkutano wa mawaziri hao utatanguliwa na mkutano wa wataalamu ambao ni wakurugenzi wa michezo kutoka nchi hizo.
Alitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Sudan, South Sudan, Eritrea, Somalia, Djibout, Mauritius Madagascar, Comoro na Seychelleys na hadi Aprili 25, 2023 nchi nane zimeshathibitisha kushiriki mkutano huo.
Katibu Mkuu Yakubu amesema kuwa katika mkutano huo ambao nchi ya Tanzania ni mwenyeji wataomba sekretarieti ya kudumu ya baraza hilo iwe iwe hapa nchini hususani jijini Arusha kwa kuwa ni makao makuu ya Jumuiya ya Afrika mashariki EAC kwa sasa sekretarieti ya baraza hilo iko yaounde cameroon.
Amesema katika mkutano huo atakuwepo kamishna wa au anayehusika na afya,masuala ya binadamu na maendeleo ya jamii,Balozi Minata Samate cessouma ambaye ataambatana na watumishi wa sekretarieti ya baraza hilo.
Katibu mkuu huyo amesema kuwa mkutano huo unafanyika katika kipindi ambacho nchi chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan umepiga hatua kubwa katika sekta ya michezo kwa kupata ushindi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa,aidha kupitia ajenda za mkutano ambazo ni uchaguziwa viongozi wa baraza la michezo,kupitia katiba ya baraza hilo na uchaguzi nchi mwenyeji sekretariet ya baraza hilo na fursa kwa nchi kujitangaza kimataifa.
Yakubu amesema kwa hapa nchi viongozi wa mashirikisho ya vyama vyote vya michezo watashiriki mkutano huo,viongozi wakuu wa Baraza la Michezo {BMT} na viongozi wakuu wa Baraza la Michezo Zanzibar{bmz} na waziri wa utamaduni,michezo na sanaa zanzibar pia atashiriki.
Amesema pia viongozi wa vyama vya soka vya nchi za kenya na Uganda nao wamealikwa katika mkutano huo lengo ni kutaka kila nchi za eac kushiriki kikamilifu mkutano huo.