NA MWANDISHI WETU, MANYARA
MKAZI wa Kijiji cha Kiperesa, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Sophia Ishuka (56) amejinyonga kwa mtandio akiwa nyumbani kwake kwa madai kuwa mimea yake imeathirika kwa kiwango kikubwa shambani kwake baada ya mvua kukosekana.
Imeelezwa baada ya kufika shambani kwake Machi 19, 2023 Sophia alikuta hali mbaya ya mimea hali iliyomsababishia kuanguka ghafla na kupoteza fahamu ambapo baaaye alizindukana kurejea nyumbani kwake.
Alipofika nyumbani kwake alieleza majirani zake mkasa na kilichompata akiwa shambani kisha kuingia ndani ya nyumba yake na kujinyonga
Diwani wa Kata ya Kiperesa Habibu Kiberenge ameelezea tukio hilo kuwa ni la kusikitisha akisema tayari ameshajulisha Jeshi la Polisi Kiteto, na kwamba kinachosubiriwa ni wao kufika kwao hapo Kijijini kwa hatua zaidi.