NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Mordena inayoongoza kwa kutengeneza dawa imesema ina uhakika kwamba dawa za saratani, magonjwa ya moyo , mishipa magonjwa yasiyokuwa na kinga na hali zingine zitakuwa tayari ifikapo 2030.
Aidha inaaminika kuwa mamilioni ya maisha yanaweza kuokolewa na chanjo hiyo mpya kwa magonjwa ikiwa ni pamoja na saratani.
Kampuni hiyo, ambayo iliunda chanjo inayoongoza ya virusi vya uviko-19 inatengeneza chanjo ya saratani ambayo inalenga aina tofauti za magonjwa.
Uchunguzi wa chanjo hizo pia unaonesha matumaini makubwa,huku baadhi ya watafiti wakisema maendeleo ya miaka 15 hayajachambuliwa katika kipindi cha miezi 12 hadi 18 kutokana na mafanikio ya uviko-19.
Dk Paul Burton, Ofisa mkuu wa kampuni ya dawa Moderna, alisema anaamini kuwa kampuni hiyo itaweza kutoa matibabu kama hayo kwa maeneo ya magonjwa ya kila aina kwa muda wa miaka mitano.
Burton amesema: “Tutakuwa na chanjo hiyo na itakuwa na ufanisi wa hali ya juu, na itaokoa mamia na maelfu, ikiwa sio mamilioni ya maisha nadhani tutaweza kutoa chanjo ya kibinafsi ya saratani dhidi ya aina nyingi tofauti za magonjwa kwa watu karibu dunia nzima”.
Pia amesema kwamba maambukizi mengi ya kupumua yanaweza kuondolewa na sindano moja kuruhusu watu walio katika mazingira magumu kulindwa dhidi ya uviko-19, homa na virusi vya kupumua (RSV) ,wakati matibabu yanaweza kupatikana kwa magonjwa adimu ambayo kwa sasa hakuna dawa.
Tiba zinazotokana na chanjon hufanya kazi kwa kufundisha seli jinsi ya kutengeneza protini ambayo huchochea mwitikio wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.
Burton amesema: “Nadhani tutakuwa na matibabu ya msingi kwa magonjwa adimu ambayo hapo awali yalikuwa hayabadiliki, na nadhani miaka 10 kutoka sasa, tutakuwa tunakaribia ulimwengu ambao unaweza kutumia teknolojia ya mRNA.