NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
JESHI la Polisi Zanzibar linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukamatwa na meno ya tembo vipande 45 katika nyumba ya kulala wageni iliyopo Fuoni kwa Mabata Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya jinai, Zubeir Chembele akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja amesema watu hao walikamatwa mwishoni mwa wiki katika nyumba ya kulala wageni iliyofahamika kwa jina la Fiori wakiwa na meno hayo katika hatua za mwisho za biashara.
Amesema uchunguzi wa shauri hilo unaendelea ambapo watuhumiwa hao majina yanahifadhiwa kwa uchunguzi zaidi lakini mmoja ni mwenyeji wa Mkoa wa Kagera na mwingine ni mwenyeji wa Zanzibar.
Akifafanua zaidi alisema Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar walipata taarifa kuhusu kuingizwa kwa meno ya tembo Zanzibar ambapo Polisi walishirikiana na kikosi kazi cha kupambana na ujangili cha Tanzania Bara (NTAP) wakaweka mtego