NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KATIKA hatua ya robo fainali Klabu ya Simba imepangwa kucheza na bingwa mtetezi wa michuano hiyo Widad Casablanca ya Morocco.
Mchezo huo wa hatua ya robo fainali dhahiri ni mfupa mgumu kwa Simba kutokana na matokeo aliyoyapata katika hatua ya makundi dhidi Raja Casablanca ambapo alikubali kupigo cha mabao 3-0 kwa Mkapa na alipokwenda Morocco akafungwa bao 3-1.
Hivyo Simba inatakiwa kujipanga sawa sawa ili kuvuka hatua hiyo dhidi ya Bingwa Mtetezi Widad Casablanca.
Katika kombe la Shirikisho barani Afrika Yanga imepangwa kukutana na Rivers United ya Nigeria ambayo katika uwanja wa nyumbani inakuwa ya moto kwa figisufigisu za nje ya uwanja na timu nyingi zinazokutana nazo hulalamikia hilo na kupoteza mchezo ikiwamo Yanga iliyowahi kukumbana na kadhia hiyo.