NA MWANDISHI WETU, GEITA
WACHIMBAJI wadogo wawili wamepoteza maisha na wengine wanne kujeruhiwa mkoani Geita katika matukio mawili tofauti likiwemo la imani Msalange (22) mkazi wa Kijiji cha Kayenze wilayani Geita kupoteza maisha baada ya kudondokewa na mwamba wakati akichimba dhahabu.
Tukio hilo limetokea Machi 29, 2023 saa 4 asubuhi katika mgodi mdogo wa dhahabu uliopo kijiji cha Shibalanga Kata ya Kaboha wilayani Nyanghwale mkoani hapa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema mchimbaji huyo akiwa kwenye shughuli zake za uchimbaji aliangukiwa na mwamba ulililosababisha wachimbaji wengine Daniel John (27), Kibacha Ally (22) wakazi wa Kilimanjaro, Hassan juma (49) mkazi wa Babati Manyara na Sospeter Lugalila (38) mkazi wa Misungwi mkoani Mwanza kujeruhiwa.