NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
KATIKA kuendelea kurejesha faida wanayoipata kwa jamii, Kampuni ya Meridianbet imewakumbuka Mama Lishe wa maeneo ya Kariakoo na Manzese jijini Dar es salaam kwa kuwapa Eproni.
Mbali ya kurejesha faida lakini pia Meridianbet imetoa Eproni hizo ili kuhakikisha wanalinda usafi na afya za wateja wao ambao ni walaji.
Eproni hizo zimetolewa Machi 30, 2023 na timu nzima ya Meridianbet.
Akizungumza wakati wa kugawa Eproni hizo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Meridianbet Matina Nkurlu amesema lengo ni kuwasaidia akina mama hao waweze kufanya shughuli zao za uandaaji wa chakula katika hali ya usafi na usalama.
Vilevile Nkurlu ameongeza kuwa itawawezesha kuvutia wateja wengi ambapo wakiona kuwa chakula kinaandaliwa katika hali ya usafi.
Kwa upande wake mmoja wa akina Mama walionufaika na msaada wa Eproni hizo, aliyejitambulisha kwa jina la Mama John amesema kuwa anawashukuru Meridianbet kwa kuwafikia nakuwaletea Eproni hizo kwani uhitaji ulikuwa ni mkubwa sana kwao lakini pia waendelee hivyo hivyo kuwafikia wananchi wote wenye uhitaji.