VATICAN CITY, VATICAN
MSEMAJI wa Kanisa Katoliki, Vatican, Matteo Bruni amesema kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amelazwa hospitalini tangu jana Jumatano Machi 29, 2023 akisumbuliwa na matatizo ya kupumua.
Taarifa iliyotolewa leo Machi 30, 2023, Msemaji huyo wa Vatican, imesema kwamba Papa ambaye ni raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 86 anasumbuliwa na tatizo la kupumua ambalo ni la kawaida na siyo Uviko 19.
Kauli hiyo imezima mijadala iliyotawala wengi wakihofu kuwa Papa amepata maambukizi ya UVIKO19.