NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MAREKANI kupitia Shirika la lake la Ushirikiano wa Kimataifa (USAID) na Serikali ya Tanzania Machi 29, 2023, zilisaini makubaliano ya miaka mitano ya msaada wenye thamani ya takriban Dola za Kimarekani Bilioni 1.1 (sawa na sh. Tril 2.5 za Kitanzania).
Chini ya makubaliano hayo, USAID itafanya Kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania kutoa msaada katika Maeneo ya Ukuaji Uchumi, Afya, Elimu, Demokrasia na Utawala bora