NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa kikosi cha Yanga kinachoongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Clement Mzize, ameamua kubadili dini na kuwa muislamu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana leo Machi 23, 2023 kupitia Runinga ya mtandaoni ya TV Quran ilibainisha kuwa mwanandinga huyo anayechipukia kwa sasa na kuwa mwiba kwa timu pinzani, amebadili dini leo mbele ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Ahmed.
Imeelezwa kuwa mchezaji huyo aliyezaliwa Januari 7, 2004 baada ya kusilimu kwa sasa anaitwa Walid Mzize, akichukua jina la Sheikh Walid ambaye ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.