Spurs wataka Tsh. Bilioni 287.5 kumuuza Kane
KUTOKANA na timu mbalimbali nchini Uingereza na nje ya taifa hilo kutaka kuimarisha vikosi kwa kununua mshambuliaji wa kikosi cha Spurs na timu ya taifa ya Uingereza, Harry Kane klabu yake imeweka kitita cha pauni milioni 100 kwa klabu inayomtaka.
Tuko tayari kumuuza kwa klabu yoyote inayotaka huduma wa mchezaji wetu Harry Kane lakini hatupo tayari kumuachia kwa gharama ya chini ya Pauni Milioni 100 (Tsh. 287,467,849,347). Kwa klabu ambayo itafikia bei hiyo ije wakati wowote tumalizane,” ilisema taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa Machi 21, 2023
Kane ( 29) ikiwa atauzwa majira ya joto mkataba wake katika klabu ya Spurs utakuwa umesalia mwaka mmoja (Times )
MANCHESTER, ENGLAND
UONGOZI wa timu ya soka ya Uingereza ya Manchester United umesema kwamba hawataiuza klabu hiyo kwa bei ya kijinga kwa mtu anayetaka kuinunua ni lazima aweke mzigo unaoeleweka na si vinginevyo.
Katika kipindi hiki ambacho klabu hiyo imewekwa sokoni matajiri mbalimbali kutoka falme za kiarabu wamekuwa wakitiririka kutaka kuichukua na mazungumzo kadhaa yamekuwa yakiendelea bila kufikia mwisho.
Hatuwezi kuiuza Man U kwa bei ya kitoto, kwa maana mtu ambaye anataka kuinunua aje na fuko la fedha, tofauti na hivyo waiche klabu yetu,” alinukuliwa mmoja wa viongozi wa timu hiyo.
Wakati hayo yakijiri Sheikh Jassim bin Hamad Al-Thani yuko tayari kutoa kitita cha Euro bilioni 5.5 (Tsh. Bilioni 12.6) ili kufanikisha kuinunua Man U. (The Mirror)
Aubameyang kutimkia Bacrcelona
MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Emerick Aubameyang, (33) yuko mbioni kurejea katika kikosi cha Barcelona msimu ujao wa majira ya joto huku maswali mengi yakiulizwa kama ataweza kuachiwa kuondoka. (Sports)
Bye bye Antonio Conte
MENEJA wa kikosi cha Tottenham Hotspur, Antonio Conte, wakati wowote huenda akaondoka katika klabu hiyo huku maswali mengi yakiwamo kwa wadau wa soka ni nani anaweza kuvaa viatu vya kocha huyo.
Tetesi zinasema wakati Conte (53) raia wa Italia akiwa mbioni kuondoka, inawezekana mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Ryan Mason mwenye miaka 31 anatarajiwa kuchukua mikoba hiyo hadi mwisho wa msimu.
Conte ni miongoni mwa makocha ambao wamekuwa na mafanikio makubwa katika klabu ambazo amepita ikiwamo Juventus, Chelsea, Inter Milan na nyingnezo (Telegraph )