NA MAGENDELA HAMISI, DAR ES SALAAM
UCHAGUZI wa viongozi wa Chama Cha Baiskeli Tanzania (CHABATA) unaratajiwa kufanyika Aprili 02, 2023 jijini Dodoma.
Ofisa Habari wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Najaha Bakari, amesema kuwa ili kukamilisha mchakato huo, fomu zimeanza kutolewa leo Machi 9 hadi 31, 2023 katika ofisi zao zilizopo Uwanja wa Benjamin Mkapa jiji Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa licha ya fomu kupatikana katika ofisi za BMT, pia zitakuwa zikipatikana kupitia yao na usahili wa wagombea wa nafasi mbalimbali unatarajiwa kufanyika Aprili Mosi.
Aidha amefafanua kuwa nafasi zinazogombewa ni Uwenyekiti, Mwenyekiti Msaidizi ambapo ada ya fomu ni shilingi 50,000, nafasi nyingine ni Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi na wajumbe watano wa Kamati ya Utendaji ambapo fomu zitatolewa kwa gharama ya sh. 30,000.