.Aiweka mguu sawa kwenda robo fainali
NA MAGENDELA HAMISI, DAR ES SALAAM
KIUNGO Mshambuliaji wa kimataifa mzaliwa wa Lusaka nchini Zambia Clatous Chama, ameendelea kuonesha umahiri wake katika kutandaza kandanda safi katika ardhi ya Tanzania na zaidi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika ‘CAFCL’ baada ya kuwalowesha Vipers FC.
Katika mchezo ambao umemalizika muda mfupi uliopita kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini, Dar es Salaam, Chama amefanikiwa kuibeba mabeba mabegani mwake yake klabu ya Simba kwa kuifungia bao 1-0 dhidi ya Vipers ya Uganda na kuendeleza rekodi ya kwa ‘Mkapa Hatoki Mtu’.
Baada ya ushindi huo katika michuano hiyo, Simba imefikisha alama sita ambazo zinawasha taa ya kijani kwa kushika nafasi ya pili baada ya Horoya FC kupoteza ikiwa nyjmbani kwa mabao 3-1 na kubaki nafasi ya tatu ikiwa na alama nne kibindoni.
Timu inayoshika mkia katika kundi lao la C ni Vipers Fc ikiwa na alama moja baada ya kutoka sare dhii Horoya na katika kundi hilo Raja Casablanca ya Morocco imekuwa ya kwanza kutinga robo fainali baada ya kushinda michezo yote minne..
Kulingana na matokeo ambayo imepata Simba sita na inahitaji kushinda mchezo ujao dhidi ya Horoya ambao utakuwa ni kama fainali kwa timu hizo mbili ili kujihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali katika michuano hiyo mikubwa Afrika.
Simba hadi sasa tayari imeshuka dimbani katika michezo minne na imepoteza miwili, ukiwamo wa kwanza wa ugenini dhidi Horoya ilipopoteza bao 1-0 na wa nyumbani ilipokubali kupigo cha mabao 3-0 dhidi ya Raja na baada ya hapo ikashinda ugenini dhidi ya Vipers kwa bao 1-0 na wapili uliochezwa jana na kuvuna alama sita kwa Vipers FC.
‘Mwamba wa Lusaka’ aibeba Simba mabegani
Leave a comment