Barcelona bado wanapambana kusaka saini ya kiungo wa kati wa Ureno, Bernardo Silva. Manchester City wapo tayari kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye mkataba wake unaisha Juni 2025, kama watapatiwa pesa kiasi cha Euro 65m (Tsh. Bilioni 143.3).
MACHESTER CITY
Man City wanataka kumsajili mlinzi wa klabu ya RB Leipzig, raia wa Croatia, Josko Gvardiol, 21 ikiwa watamuuza mlinzi wa Hispania, Aymeric Laporte, 28, ambaye anaivutia klabu ya Paris St-Germain.
Pia klabu hiyo inamuwania kiungo wa kati wa Ufaransa, Adrien Rabiot, 27 ambaye anaandaliwa kuwa mbadala wa mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani, Ilkay Gundogan, 32 ambaye anaweza kutimkia Barcelona. Wachezaji wote wawili mkataba wao unamalizika msimu wa joto.
TOTTENHAM
Tottenham wanataka angalau Pauni Milioni 100 za Uingereza (Ts. Bilioni 281.6) ikiwa watamuuza mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, 29, ambaye amebakiza miezi 15 katika mkataba wake wa Spurs, msimu huu wa joto.
MANCHESTER UNITED
Mashetani wekundu wa jiji la Manchester wanasaka saini ya kiiungo wa kati wa Uholanzi, Frenkie de Jong. Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anatamani kubaki kwenye klabu yake ya Barcelona.
BRIGHTON
Kiungo wa kati wa Ecuador, Moises Caicedo huenda akatia saini mkataba mpya na klabu yake ya Brighton japo anawaniwa na klabu nyingine za Ligi Kuu ya Uingereza.
CHELSEA
Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Ureno, Joao Felix, 23, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Blues kutoka Atletico Madrid, na kiungo wa kati wa West Ham ya Uingereza, Declan Rice, 24, msimu wa joto na wanapanga kuwauza wachezaji watano ili kusaidia kufidia gharama hiyo.
AC MILAN
AC Milan inamtaka kiungo wa kati wa Chelsea, Ruben Loftus-Cheek na italazimika kulipa Euro 25m (Tsk. Bilioni 70.4) ili kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.
BARCELONA
Kiungo wa kati wa Ivory Coast, Franck Kessie amekuwa akihusishwa na kutaka kuondoka Barcelona lakini klabu hiyo ya Hispania haina nia ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 msimu wa huu wa joto.
LIVERPOOL
Mshambuliaji wa Brazil, Roberto Firmino bado hajafanya mazungumzo na klabu nyingine yoyote kabla ya kuamua kuondoka Liverpool wakati mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto, kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31.