NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
RAIS Samia Suluhu Hassan amewataka Mawaziri kuacha kuajiri Maofisa Habari binafsi katika wizara zao.
Aidha Rais Samia amewataka Mawaziri kutumia vitengo vya Habari vya Wizara kutoa taarifa za serikali
Sambamba na hilo, Rais Samia amezitaka Wizara kujibu kauli za upotoshaji zinazotolewa na wanasiasa kuhusu utendaji wa Serikali.
“Najua kila Wizara ina kitengo cha habari, vitengo hivi vinatumikaje, vipo tu vimekaa havifanyi kazi lakini bado mawaziri mmeajiri maafisa wenu habari binafsi wa kutoa taarifa zenu na si taarifa za Serikali, sasa hili tukarekebishe”, amesema Rais Samia.
Rais ametoa maagizo hayo leo Machi 02, 2023 katika mkutano wa faragha wa Mawaziri na Manaibu Waziri uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (AICC) uliofanyika Jijini Arusha.