NA STEPHANO MANGO, SONGEA
MKUU wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile ametoa siku 14 kwa Maofisa Watendaji Kata, Mitaa na Maofisa Elimu Kata kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kuwapata wanafunzi 469 wasioripoti shule ikiwa wanafunzi 6343 waliochaguliwa kujiunga kidato kwanza 2023 kati ya hao ni Wanafunzi 5874 wameripoti shule.
Amewataka kutumia mbinu shirikishi jamii ili kufanikisha kuwapata wanafunzi wote ambao bado hawajaripoti pamoja na kubaini changamoto ambazo zinapelekea Mwanafunzi kutoripoti shule kwa wakati husika.
Aidha, ametoa rai kwa wataalam hao kuwajibika kila mtu katika eneo lake na ameahidi kutoa zawadi kwa Mtendaji yeyote atakaye fanikisha kwa asilimia 100 kusimamia zoezi la wananfunzi wasioripoti shuleni.
Kauli hiyo imetamkwa jana katika kikao kazi cha Maofisa Watendaji Kata 21, Maofisa Watendaji wa Mitaa 95, Maofisa Elimu Kata 21, Wakuu wa Idara kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Wasichana Songea kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wameripoti na wasioripoti Manispaa ya Songea.
Ndile amewataka Watendaji wa Serikali za Mitaa kuandaa Mpango shirikishi ambao utatekelezeka katika kufanikisha utoaji wa chakula shuleni ambapo amesema ni asilimia 63 za shule ambazo zinatoa chakula kwa wananfunzi wakati wa masomo.
Kwa upande wa Ofisa Elimu Sekondari Janeth Moyo amesema Manispaa ya Songea imeweka Mkakati wa kuhakikisha wanatumia mbinu mbalimbali ikiwemo na sheria ndogo ili kufanikisha kuwapata wanafuzi wasioripoti