NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
BENKI ya Standard Chartered Tanzania imetoa ripoti yake ya kwanza ambayo inaonesha mchango wa benki hiyo katika kuchochea maendeleo endelevu kwa mwaka 2022 iitwayo ‘Here for good a sustainable future for Tanzania’.
Ripoti hiyo inaangazia juhudi za benki na mafanikio yaliyopatikana katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kampuni imechangia maendeleo kwa watanzania kupitia nguzo tatu za maendeleo za benki, uwekezaji wa fedha katika miradi endelevu, kampuni inayowajibika, na ujumuishaji.