NA REBECA DUWE , TANGA
JESHI la Polisi mkoani Tanga limetoa tahadhari ya matukio ya ukatili wa kijinsia katikati maeneo mbalimbali jijini hapa
Tahadhari hiyo imetolewa na Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Tanga Henry Mwaibambe wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo aliwataka wananchi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa vitendo hivyo vinaishi kwenye jamii yetu hususani kwa watoto na wanawake
Sambamba na hayo amesema aliwaonya wale wote wenye dhamira ovu ya unyanyasaji kwa watoto na wanawake kwenye jamii ambapo suala hili limekuwa kinara juu ya uvunjifu wa maadili waliyokuwepo hapo awali katika Taifa la Tanzania
Aidha amebainisha kuwa Jeshi la Polisi limeweka mikakati madhubuti Ili kuhakikisha kuwa jamii ipo salama kwa kutokomeza vitendo Kwa ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji na ulawiti kwa watoto hivyo limeomba kutoa ushirikiano kwa wananchi wote pasipo kuangalia dini,cheo au wadhifa wa mtu na yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Sambamba na hayo amewataka wazazi na walezi wote kuwalinda watoto kwa kufuatilia mienendo yao Ili kubaini changamoto wanazokumbana nazo kwenye jamii kwa kuwapatia elimu kuhusiana na vitendo viovu ili kujikinga na matukio ya ubakaji na ulawiti .
” Wazazi na walezi wote niwaombe kuwa makini sana kuwajali watoto wenu kwa kufuatilia mienendo yao mwanzo mwisho ili kuepukana na vishawishi vitakavyowapelea watoto hao kujiingza kwenye majanga lakini pia msiishie tu tuwanunulia vifaa vya shule na ada za masomo ya ziada ukaona kuwa umemaliza bali unatakiwa pia kujua mtoto alifika shule, maendeleo yake yapoje na hata wanapoenda sehemu nyingine kama nyumva za ibada hakikisha mtoto wako yupo kwenye mazingira mazuri”.alisema Mwaibambe.
Wakizungumzia juu ya tahadhari hiyo kwa nyakati tofauti viongozi vya dini Mchungaji Lewis Shemkala na Mchungaji Charles Kakai wa kanisa la Kiinjili la kilutheri Tanzania( KKKT )Dayosisi ya Kaskazini Mashariki wamesema kuwa utandawazi umechangia kwa asilimia kubwa kuwepo kwa vitendo vya ukatali katika jamii hivyo ni vyema jamii ikapewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.