NA MWANDISHI WETU, TANGA
MMOJA wa watuhumiwa 8 waliokamatwa wakidaiwa kuiba mali za abiria waliopoteza maisha katika ajali iliyohusisha gari ya kubeba mizigo aina ya Fuso na Costa lililokuwa likisafirisha mwili kwaajili ya maziko wilayani Rombo na kusababisha vifo vya watu 20 amekutwa amejinyonga kwenye shamba lake mkoani hapa.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba, mtuhumiwa huyo ni yule ambaye wakati wa upekuzi nyumbani kwake alikutwa na baadhi ya vitu vikiwemo simu, begi na nguo zinazosadikiwa kuibiwa eneo la ajali.