NA MWANDISHI WETU
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Serikali haitavumilia kuwepo kwa mitandao na tovuti zinazokiuka maadili na desturi za Kitanzania.
Nape aliyasema hayo jana Alhamisi, Februari 22, 2023 alipokuwa anajibu maswali wakati akishiriki mjadala kwenye mtandao wa Clubhouse.
Waziri huyo mwenye dhamana ya mawasiliano alisema wizara yake inavyo vifaa vya kutosha na vya kisasa vinavyoweza kuzima mitandao yote na tovuti zinazokinzana na maadili ya Kitanzania.
Alipoulizwa kama serikali inahusika kuzima App ya Mange Kimambi, Nape alisema; Ukiona huupati mtandao ambao zamani ulikuwepo na mtandao huo unakiuka maadili ya Kitanzania basi fahamu serikali imeudhibiti ili kulinda maadili yetu.