NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
NABII Mkuu wa Kanisa la Ngurumo ya Upako lililopo Kisongo jijini hapa Dk GeorDavie ametoa wito kwa watumishi kupunguza wingi wa ibada makanisani na kuwaacha watu wakafanye kazi.
Kauli hiyo ameitoa leo februari 22 jijini hapa katika hafla iliyoandaliwa na waumini wake kwaajili ya kumpongeza Nabii Mkuu kuadhimisha mwaka mmoja tangu alipoanza kutoa misaada mbalimbali katika jamii.
“Nitoe hamasa kwa watumishi kupunguza ibada nyingi makanisani na badala yake waache waumini wakafanye kazi” amesisitiza Nabii Mkuu Dk GeorDavie