NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini Hussain Ahmad Al – Homaid katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali hususani ya kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Qatar ambapo Balozi Fatma amemhakikishia Balozi wa Qatar kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Qatar kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo viwanda, biashara na uwekezaji.